18 Mei 2025 - 19:26
Mwandishi wa Habari wa ABNA Aibuka Mshindi katika Tamasha la 10 la Vyombo vya Habari la Abu Dharr katika Mkoa wa Qom

"Mohsen Saberí" ametangazwa kuwa mmoja wa washindi wa Tamasha la 10 la Vyombo vya Habari la Abu Dharr katika mkoa wa Qom.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la AhlulBayt (a.s) - ABNA - Katika hafla ya kufunga Tamasha la 10 la Vyombo vya Habari la Abu Dharr katika Mkoa wa Qom, iliyofanyika leo Jumapili asubuhi katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu cha Ma'arif Islamiya mjini Qom, mmoja wa waandishi wa habari wa Shirika la ABNA alitunukiwa cheti cha Heshima kwa kushinda nafasi ya juu katika kipengele cha klipu na ripoti ya video.

Kwa mujibu wa taarifa ya sekretarieti ya tamasha hilo, Mohsen Saberí, Mwandishi wa Habari wa ABNA, alipata nafasi ya tatu kwa kuwasilisha kazi bora katika kipengele cha klipu na ripoti ya video katika Tamasha hilo la 10 la Mkoa wa Qom.

Mwandishi wa Habari wa ABNA Aibuka Mshindi katika Tamasha la 10 la Vyombo vya Habari la Abu Dharr katika Mkoa wa Qom

Pia, katika sehemu ya hafla hiyo, Hassan Sadraei Aref, Mkurugenzi wa Shirika la Habari la ABNA, alitunukiwa tuzo ya kumbukumbu na cheti maalum kama ishara ya kuthamini mchango wa shirika hilo katika kuunga mkono uendeshaji wa Tamasha la 10 la Vyombo vya Habari la Abu Dharr katika Mkoa wa Qom.

Inafaa kutajwa kwamba tamasha hili lililoandaliwa na Basiij ya Wanahabari wa Mkoa wa Qom, lililenga kuthamini juhudi za wanahabari wa mkoa huo, na limepokelewa kwa mwitikio mkubwa kutoka kwa wadau wa vyombo vya habari mjini Qom.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha